CEO wa FKF Michael Esakwa |
Kenya haitacheza na Tanzania bara mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo kama ilivyoarifiwa mapema.
Harambee Stars ilikuwa ikijipanga kuikabili Kilimanjaro Stars katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujiandaa kwa michuano ya Chalenji ya Cecafa ambayo itafanyika nchini Kenya.
Katika barua iliyotumwa shirikisho la soka la Tanzania TFF na kuthibitishwa na afisa wa FKF Michael Esakwa, imeelezea sababu za kuahirishwa kwa safari ya Harambee Stars kuja Tanzania na mwendelezo wake.
Taarifa hiyo imenukuliwa ikisema
“Kwa huzuni kubwa tunaliarifu shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kuwa hatutaweza wa kucheza mchezo huo kimataifa wa kirafiki uliopangwa kuchezwa Novemba 19.”
"Tunaomba radhi kwa usumbufu utakao jitokeza. Tunaangalia uwezako kwa tarehe za mbele”.
Taarifa hii inakuja siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Chalenji na Kenya bado haijatangaza orodha ya wachezaji wake kuweza kucheza mchezo huo wa Jumanne na Tanzania.
Kenya itakutana na Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo Novemba 27.
Kocha wa Harambee Adel Amrouche anatarajiwa kuweka wazi majina ya wachezaji wake kujiandaa na michuano hiyo ambapo wamepoteza heshima yao ya taji kwa kipindi kirefu na hiyo fursa nyingine ya kurejesha heshima hiyo.
No comments:
Post a Comment