Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 5, 2013

AHLY WANAJIPA MOYO WA KUTWAA TAJI KWENYE ARDHI YA MISRI.



Licha ya kufanikiwa kusawazisha na kupata sare ya bao 1-1 na kuepuka kichapo cha uwanja wa nyumbani kutoka kwa Al Ahly ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa vilabu bingwa Afrika Jumamosi usiku, Kocha wa Orlando Pirates De Sa anaamini kuwa ina kila sababu ya kutwaa taji hilo.
Amenukuliwa baada ya mchezo akisema 
"Bado tuna nafasi ya kupigania taji mbele ya Wamisri".

"Tumeonyesha uwezo wa kufanya hivyo na tunaamini tutabadilisha hali ya mambo Huko Misri
"Itakuwa ngumu sana lakini hakuna wasiwasi na hilo lakini tunakwenda kushinda kule."
Thabo Matlaba alifunga goli la kusawazisha katika dakika za lala salama za nyongeza baada ya Mohamed Aboutrika kufunga goli la uongozi kwa wageni kunako dakika ya ya 45 kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja(free-kick).
Wakati fainali ikiwa inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, Ahly wananafasi ya faida ndogo ya sare ya ugenini huku Buccaneers wakiwa bado wanashukuru bao la Matlaba la dakika za  mwisho.

No comments:

Post a Comment