Pages

Saturday, October 12, 2013

YANGA YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1


Asante Ngassa

Chukua tano kwanza ....Asante!!
Kikosi cha Kagaera Sugar kilichoanza

Kikosi cha Yanga



Dakika ya 2 Mpira ukirushwa kama kona na Kipa kuupangulia kwa adui na Hatimaye Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa akafanikiwa kuipatia bao na hapa walikuwa wanashangilia bao hilo. Mpaka Mapunziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar. Habari na www.bukobasports.com

Wachezaji wa Yanga wakishangilia Baada ya kupata bao kupitia kwa Mrisho Ngassa



Patashika Uwanjani..
Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Kipindi cha pili dakika ya 49 Godfrey Wambura akaisawazishia bao timu yake na kufanya 1-1 na mtanange Kuchangamka sana kuliko kipindi cha kwanza..

Dakika ya 60 Hamis Kiiza akaiongezea bao Yanga na kufanya 2-1 Dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.Hakuna kwenda popote!!

Kagera Sugar wakishangilia  baada ya kusawazisha bao dakika ya 49.

Mchezaji wa Kagera akitafuta wenzake kuwapa mpira kipindi cha pili

Mashabiki walijitokeza sana
KAZI NZURI: Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kupata bao la pili na la ushindi

wachezaji wa Yanga wakimpongeza Mwenzao Kiiza baada ya kuwapatia bao la ushindi

Safi...ndugu yangu Yanga sasa tunapanda...
Nyomi ilisheeni
Kiiza akipongezwa na Mrisho Ngassa

Patashika kwenye goli la Yanga
Kiongozi wa Yanga nae akiojiwa kuhusu mtanange huo

No comments:

Post a Comment