Pages

Thursday, October 24, 2013

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA MCHEZO WA MAGONGO YAKABILIWA NA UKATA




Timu ya Taifa ya mchezo wa magongo ya wanawake inakabiliwa na ukata unatishia kushindwa kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 18 hadi 24 mwaka huu.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO kwenye Uwanja wa Karume uliopo Ilala, Dar es Salaam, kocha wa timu hiyo Muitaliano Valentine Quarente alisema kuwa timu ipo vizuri na imejiandaa vya kutosha na wachezaji wana ari.

"Timu ipo vizuri na wachezaji wana ari ya mashindano kwani ni mara ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa ila ukata ndio unaotutia unyonge", alisema Valentine.

Mashindano hayo yatafanyika katika viwanja vya City Park jijini Nairobi, na watacheza na Misri, Afrika ya Kusini, Kenya na Ghana

Timu ya magongo ya wanawake inaundwa na wachezaji 17 na imekuwa ikicheza michezo ya kirafiki na timu za wanaume, na leo imecheza na timu ya Magongo ya wanume ya Zanzibar na kufungwa 4-0.

Pia amekishukuru chama cha mchezo wa Magongo cha Ilatia, Tulime Onlis, COPE, Pepsi na watu mbalimbali kwa michango yao katika kufanikisha kambi ya timu hiyo

No comments:

Post a Comment