Pages

Sunday, October 20, 2013

TBL YATOA MILIONI 7.2 KWA WASHINDI WA MITUMBI KIGOMA

Katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma, Joshua Elisha(kulia) akimkabidhi mwakilishi wa kikundi Makila fedha taslimu Shilingi 900,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya bio za mitumbwi yanayodhaminiwa na Bia ya Balimi Extra Lager, Kanda ya Ziwa kwa ngazi ya mikoa Mkoa wa Kigoma yaliyofanyika katika ufukwe wa Kibirizi mwishoni mwa wiki

Na Mwandishi Wetu.Kigoma
KAMPUNI ya Tanzania Breweries Limited (TBL)  imetoa kiasi cha shilingi milioni 7.2 katika shindano la mbio la wasooza mitumbwi kwa kipindi cha mwaka 2013 lililofanyika katika Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma.

Akikabidhi fedha hizo kwa washindi wa shindano hilo, katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma bw. Joshua Elisha amewataka washindi hao kutumia vyema fedha walizozipata katika kuinua uchumi wa maisha yao.

Amesema kuwa kupitia michezo hiyo inayofanyika kila mwaka mkoani Kigoma ni njia mojawapo ya kuwaweka watu pamoja kwa kushirikiana kuboresha maslahi yao pamoja na  biashara zao kwa kununua vifaa vya kisasa vya  kuvulia mazao ya samaki na dagaa.

“Fedha hii isiwe sababu ya kuanza malumbano ya kikundi ni lazima kama kikundi kufanya uwekezaji kwa kuboresha zana za kuvulia na kuacha tabia ya kutumia zana ambazo haziruhusiwi kisheria kufanyia shughuli za uvuvi, halafu faida itakayo patikana ndio kila mmoja anufaike kupitia uwekezaji uliofanyika awali” amesema bw. Elisha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  mwenyekiti wa chama cha mbio za mitumbwi Taifa bw. Richard Mgabho na mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma bw. Huseni Hatibu wamesema kuwa mashindano hayo ni endelevu na washindi wa mkoa wa Kigoma watashiriki shindano  la Kikanda jijini Mwanza ambapo waliwataka washindi hao kufanya mazoezi kwa bidii na kuacha tabia ya kutumia mbinu za kishirikina.

Wamesema kuwa katika shindano la ukanda wa ziwa mikoa itakayo shiriki ni pamoja na Kagera, Msoma, Kigoma pamoja na jiji la Mwanza ambapo donge nono litatolewa kwa mshindi atakaye shinda katika shindano la kanda ya ziwa.

Aidha washindi hao kwa upande wa wanaume ni kikundi cha Makila kimeibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia shilingi laki tisa, mshindi wa pili beach Boy Katonga laki saba, watatu Katonga A kapata laki tano na mshindi wan nne  Katonga Beach kapata laki nne,  huku mshindi wa tano hadi kumi wamepata shilingi laki mbili na nusu kati ya vikundi 23 vilivyo shiriki ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tatu watashiriki shindano la kikanda jijini Mwanza hivi karibuni.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni kikundi cha Mwamgongo kapata laki saba, wa pili Remba kapata laki sita, watatu Best Gerezi kapata laki nne na wan ne Tanganyika kapata laki tatu huku mshindi wa tato hadi kumi wamepata kali mbili kila kikundi kati ya vikundi 14 vilivyo shiriki ambapo msindi wa kwanza na wapili nao watashiriki shindano la kikanda.

Hata hivyo mwakilishi wa kampuni hiyo Mkoa wa Kigoma bw Kasile Kasile amesema kuwa lengo la kampuni  kuweka mashindano hayo ni kutaka kurudisha fadhila kwa wateja wao ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi na kuboresha maisha ya wavuvi nchini sambamba na kushiriki katika miradi ya kimaendeleo

No comments:

Post a Comment