Pages

Wednesday, October 9, 2013

TAMBWE AIBEZA YANGA



MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, Amisi Tambwe, amebeza na kusema Yanga haina tofauti na timu ambazo wamekutana nazo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tambwe anaongoza kwa ufungaji akiwa amepachika mabao 8 katika mechi saba alizocheza, akiwa katika kikosi hicho cha Simba, kinachonolewa na Kocha Abdallah Kibadeni.

Akizungumza na DIMBA jana jijini Dar es Salaam, Tambwe alisema timu za Tanzania hazina tofauti kubwa katika viwango vya wachezaji, hali anayoifananisha na Yanga, kama timu ambazo tayari walishakutana nazo na kuwafunga.

Alisema hakuna timu rahisi katika ligi ya nchi yoyote, huku akizisifu Mtibwa Sugar, Mbeya City na Rhino Rangers kuwa ni timu tishio ambazo wachezaji wake hupambana kuliko Yanga.

 “Sijawahi kuiona kwa sasa Yanga, ninaiheshimu kama timu nyingine, ila ninachokiona Yanga haina tofauti kubwa na timu nyingine tulizokutana,” alisema.

No comments:

Post a Comment