Pages
▼
Saturday, October 19, 2013
TAMBO ZA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA ZINAONGOZWA PIA NA REKODI
1. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba hapo tarehe 07/06/1965 pale ipoibugiza Simba bao 1-0 mfungaji akiwa ni Mawazo Shomvi katika dakika ya 15 ya mchezo.
2. Yanga ndiyo timu ya kwanza kuibamiza Simba kichapo cha paka mwizi cha 5-0 hapo tarehe 01/06/1968. Kwa kipindi cha takribani miaka 9 hivi Simba ilikuwa ikijipanga kulipa kisasi hicho na ilipofika tarehe 19/07/1977 iliibamiza Yanga kipigo kikali zaidi cha 6-0.
3. Abdallah Kibadeni wa Simba ndiye mchezaji pekee aliyeweza kupiga bao 3 (hat trick) katika mapambano ya watani siku ya kifo cha karne cha Yanga cha bao 6-0 siku ya tarehe 19/07/1977. Kipigo hiki hakijalipwa na Yanga hadi leo.
4. Simba kwa mara nyingine tena iliibamiza Yanga kipigo kikali cha bao 5-0 siku ya tarehe 06/05/2012. Kipigo hiki ni malipo kwa Yanga kwa kipigo kama hicho cha tarehe 01/06/1968.
5. Hadi sasa watani Simba na Yanga wamecheza mapambano 109. Mapambano 30 yaliisha kwa sare au suluhu bila kutambiana. Yanga imefanikiwa kushinda mapambano 43 huku Simba ikitamba katika mapambano 36. Hadi sasa Simba inadaiwa na Yanga mapambano 7 ya kushinda.
6. Hadi sasa Yanga imefanikiwa kuifunga Simba mabao 140 huku Simba ikizifumania nyavu za Yanga mara 132. Simba inadaiwa na Yanga mabao 8.
7. Takwimu katika vipengele 5 & 6 hapo juu zinaungwa mkono na mataji ya ubingwa wa ligi kuu ambapo Yanga imefanikiwa kuchukua ubingwa mara 24 huku Simba ikishinda mataji mara 18.
No comments:
Post a Comment