LONDON, England
NI jambo la kawaida kwa wachezaji kung’ara
kipindi fulani na kujizolea sifa nyingi katika tasnia hiyo ya soka hadi
wanastaafu.
Hata hivyo bahati hiyo imekuwa
ikiwakuta wachezaji kutokana na baadhi yao kung’ara na kisha wakatoweka kwenye
ramani hiyo ya soka.
Katika makala haya tunajaribu kuangalia
wachezaji watano ambao waling’ara wakiwa kwenye Ligi Kuu ya England kabla ya
kutoweka kwenye ulimwengu wa soka.
1. Alex Song
Baada ya kujiimarisha katika nafasi
ya kiungo katika timu ya Arsenal na huku
akionekana kuelewana vizuri na Robin van Persie, raia huyo wa Cameroon alijinadi jina lake na kuwa kiungo mkabaji
mwenye kiwango cha hali ya juu katika timu hiyo ya Gunners.
Lakini baadaye zikawapo taarifa za
kwamba anataka kuitema Arsenal na baadaye Song akajiunga na Barcelona kwa ada
ya pauni milioni 17.
Hata hivyo tangu ajiunge na vinara
hao wa soka wa Catalan, Song hajawahi kutakata na watu tayari wameshaanza kusahau
mtu anayeitwa Song.
Inaelezwa kwamba, kwa sasa kuna
uwezekano ukamuuliza mtu yeyote kama amewahi kusikia mtu anayeitwa Song,
pengine ukaambulia jibu la Song ndiye mtu gani?
2. Ibrahim Afellay
Huyo ni mchezaji mwingine ambaye
alikuwa tishio kabla ya kujiunga na Barcelona na kwa sasa amesahaulika.
Alijiunga na timu hiyo kwa ada ya dola
milioni 3 na akafanikiwa kumaliza msimu mmoja akiwa na timu hiyo ya La Liga, ambapo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu
Bingwa Ulaya na Ligi Kuu.
Hata hivyo baadaye alitoweka kwenye
medani ya soka na kutokana na majeraha yaliyomfanya kukaa kando ya kikosi hicho,
hakuweza kukomaa na kazi kama alivyokuwa mwanzo.
Kutokana na hali hiyo, msimu huu
timu hiyo imempeleka kwa mkopo katika timu ya Schalke, lakini nako mambo
yanaonekana kumuaribikia baada ya kukumbwa na matatizo ya misuli ya nyama za
paja ambayo yatamfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili.
Inaelezwa kwamba, kwa sasa nyota
huyo huwezi kumkumbuka endapo hautakuwa uwanjani.
3. Salomon Kalou
Nyota huyo wa zamani wa Chelsea, alipangwa kwenye mechi mbili za Klabu
Bingwa Ulaya, moja ikiwa ni ile ambayo timu hiyo ilifungwa na ya pili ambayo
timu hiyo iliweza kutwaa ubingwa.
Licha ya kuwa kati ya wachezaji
waliopiga mashuti ya penalti, pia ni kati ya walioifanya Chelsea kushindwa.
Baada ya kuonekana kwa mara ya
mwisho katika kikosi cha Blues na kutwaa
nacho ubingwa, baadaye aliruhusiwa
kwenda kujiunga na timu ya Lille ya nchini Ufaransa.
Hata hivyo tangu atimke, naye
amekuwa miongoni mwa wachezaji waliosahaulika na itamlazimu alazimishe kurejea
kwenye michuano ya Ligi Kuu ya England, endapo atataka kurudisha jina lake
kwenye ramani ya soka.
4. Florent Malouda
Nyota huyo pia ni kati ya wachezaji waliotoa mchango mkubwa Chelsea na
timu ya Taifa ya Ufaransa.
Nyota huyo aliwahi kucheza fainali
za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Ujerumani, jambo ambalo analiona kama tunu kwake katika
kazi yake ya kusakata kandanda.
Hata hivyo katika kipindi cha mwisho
Chelsea alishindwa kupangwa kwenye kikosi cha kwanza na badala yake akawa
akitumika kama mchezaji wa akiba.
Kwa sasa Malouda anasakata kandanda
katika timu ya Trabzonspor ya nchini
Uturuki na mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 33, amekuwa kati ya
wachezaji waliosahaulika.
5. Aleksandr Hleb
Katika hatua nyingine, unaweza
kumuelezea nyota huyo kuwa alikuwa mahiri kwenye kikosi cha Arsenal na mchezaji
bora kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Belarus, kabla ya kujiunga na Barcelona
ambapo alitumia muda mwingi akisugua benchi baada ya kuanzishwa kikosi cha
kwanza mechi tano tu.
Baada ya kuondoka Barcelona, alitumia muda
mwingine wa miaka minne akichezea klabu sita tofauti, lakini akashindwa
kutengeneza jina lake.
Kwa sasa nyota huyo anachezea timu
ya FC Bate Borisov na amekuwa akipondwa na mashabiki wa Arsenal wakimueleza
kuwa asingepaswa kuhama ili aweze kufanya makubwa.
No comments:
Post a Comment