Miss Tourist Tanzania 2013 Hadija Said akiondoka uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere |
Rais wa Miss Utalii Chipungahelo akimkabidhi cd pamoja na vipeperushi vya hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuitangaza hifadhi hiyo akiwa huko Equtorial Guinnea |
Miss Tourist 2013 Hadija Said (kushoto) akiwa pamoja na mrembo mwenzake Theresia Kimolo aliymsindikiza |
MREMBO wa Utalii Tanzania 2013 (Miss Tourist Tanzania 2013)
Hadija Said ameondoka nchini leo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya urembo
ya dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Equatorial Guinnea
Mashindano hayo ya Miss Utalii yanatarajiwa kufanyika Otoba
12, mwaka huu kwenye mji wa Malabo
na jumla ya nchi 126 zinatarajiwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye Uwanja wa
ndege wa Mwalimu Nyerere, mrembo Hadija Saidi alisema anaamini anakwenda
kuipeperusha bendera ya Tanzania
vyema kama warembo wenzake waliotangulia
kushiriki katika fainali hizo za dunia.
“Naamini nakwenda huku na nitarudi na taji kama
walivyofanya warembo walionitangulia”, alijigamba Hadija.
Pia aliishukuru mamalaka ya hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro
kwa kudhamini safari yake na anaamini anakwenda kuitangaza vyema hifadhi hiyo
ambayo ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia akiwemo Nyati mweupe aliyeonekana
hivi karibuni katika hifadhi hiyo.
Mashindano ya Miss Utalii yalianza nchini mwaka 2004 hadi 2007 na yalisimama kwa
miaka kwa miaka mitano hadi yalipokuja kufanyika tena mwaka huu mkoani Tanga na
mara zote kila mwakilishi anayewakilisha nchini anarudi na taji.
No comments:
Post a Comment