Pages

Sunday, October 13, 2013

MCHEZO WA KAGERA SUGAR NA YANGA WAINGIZA MILIONI 20.5/ KAITABA.


Kikosi cha Yanga kilichoanza kucheza na Kagera Sugar 
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana jioni  kati ya wenyeji, Kagera Sugar na Yanga SC umeingiza kiasi cha Sh. Milioni 20. 5, wakati kila klabu imepata mgawo wa Sh. Milioni 4.9.Taarifa kutoka Chama cha Soka Kagera (KRFA) usiku huu, imesema kwamba jumla ya Sh 20, 525,000 zimepatikana na kila timu imepata Sh. 4,907,000.
Katika mchezo huo, ambao Yanga SC imeibuka na ushindi wa 2-1, Sh. 3,139,320 ni makato ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), gharama za Uwanja Sh. 2,495,000 na gharama za mechi Sh. 1,497,000.
Makato mengine ni mgawo wa Kamati ya Ligi Sh. 1,497,000, KRFA 582, 100 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepata Sh. 748,543.

No comments:

Post a Comment