Pages

Friday, October 18, 2013

KARAMA NYILAWILA NA SADO PHILEMON SASA KUPIMANA UBAVU NOVEMBA 3


KALAMA NYILAWILA
MPAMBANO wa masumbwi uliokuwa uwakutanishe ya Bondia Kalama Nyilawila na Sado Philemon  uliokuwa uchezwe Oktoba 20 jumapili katika uwanja wa CCM Mwijuma Mwananyamala umeahirishwa kupisha mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika katika uwanja wa Taifa

Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe 'amesema mpambano huo umeahirishwa kupisha mchezo wa sSmba na Yanga kwa kuwa mashabiki wa mpira ndio mashabiki wa mchezo wa masumbwi hivyo kwa sasa mpambano huo utafanyika Novemba 3 katika ukumbi huo.
Mapambano mengine ambayo yatakuwepo ni Mwaite Juma na Shadrack Ignas, nae bingwa wa zamani wa bantam  Ajibu salum atapimana ubavu na Martin Richard, huku  Mbena Rajab atazipiga na Godwin Mawe.
 
Ibrahim class 'King Class Mawe ' atachapana na Rashid Ali, Hassan Kiwale (Moro best) na Harman Richrd, Kasim Chuma na Shaban Manjoly, mdogo wake Francis Miyeyusho Yona miyeyusho  atacheza na Julias Thomas, Abdalla ruwanje na Bakari Zoro pia kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa Mwananyamala sokoni  Joseph Stanslaus (amita au jose mawe) na mbabe wa Manzese sokoni  Shaban Seif (body kitongoji).
 
Pambano lililojaa vituko na mbwembwe kwa mabondia hawa, nae  Yasin Omari  atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na mapambano  mengine kadhaa ya vijana wadogo wenye vipaji  vya mchezo wa ngumi. Mapambano haya yote yameandaliwa na Ibrahim Kamwe wa bigright promotion  kwa kusindikiza pambano la ISSA OMAR (peche boy) atakaezipiga  na  ATHONY MATHIAS katika pambano la raundi nane,\.
 
SADO PHILEMON    atakaezipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito wa middle kutafuta mshindi  wa atakaepigana na Thomas Mashali katika pambano la ubingwa wametakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mpambano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala A

No comments:

Post a Comment