Pages

Monday, October 21, 2013

GYAN AENDELEZA REKODI YA MABAO UAE.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan ameendelea kuwa katika kiwango cha juu baada ya kufikisha mabao 60 katika Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu maarufu kama Pro League. Gyan ambaye ambaye ni nahodha wa Ghana alifanikiwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 5-1 iliyopata timu yake ya Al Ain dhidi ya Dubai na kufikisha mabao saba katika mechi nne za ligi alizocheza msimu huu. Wiki iliyopita Gyan alifunga mabao mawili katika ushindi mnono wa mabao 6-1iliyopata Ghana katika mchezo wa mtoano wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Mabao hao matatu aliyofunga Gyan katika Pro League yanamfanya kufikisha jumla ya mabao 60 katika mechi 44 alizocheza katika misimu miwili ambayo amekuwa huko.
Asamoah Gyan

No comments:

Post a Comment