Pages

Tuesday, October 8, 2013

GUS POYET ATEULIWA KUWA MENEJA MPYA WA SUNDERLAND KWA MIAKA 2

first interview gus poyetGus Poyet kocha mpya Sunderland
KLABU ya Sunderland imemteua Kocha wa zamani wa Brighton Gus Poyet kuwa Meneja mpya wa Klabu hiyo ya Sunderland leo Jumatano kuonoa timu kwa miaka matatu.
Sunderland, ambao wako mkiani kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na Pointi 1 katika Mechi 7, walimtimua Paolo Di Canio hapo Septemba 22 baada kudumu kwa Miezi 6 akiongoza Mechi 13 tu.


Klabu hiyo ambayo inajulikana kama "The Black Cats " inashikilia mkia katika ligi kuu ya Premier na ilimpiga kalamu Paolo Di Canio mnamo mwezi wa September baada ya kuhusika na mechi 13 tu.
Ataungana na wasaidizi wake za zamani wa Brighton Mauricio Taricco na Charlie Oatway."nina hamu ya kuwathibitishia uwezo wangu mashabiki--ninataka wawe na imani kwa sababu tunahitaji kushikamana " Poyet, mwenye umri wa miaka 45, ameiambia wavuti wa klabu hiyo.

"Nadhani msingi wa mafanikio yangu katika mechi za nyumbani Brighton ni uhusiano wangu na mashabiki, --na naweza kuona hali hiyo hiyo hapa ,"aliongeza Poyet, ambaye alipigwa kalamu na Brighton mnamo mwezi wa Juni.

"ni changamoto kubwa lakini inanipa motisha na nashukuru kwa kupata fursa hii ya kuongoza katika ligi kuu"
Poyet ambaye ni mchezaji wa zamani wa taifa wa timu ya Uruguay atakua meneja wa sita wa Sunderland katika kipindi cha miaka mitano.
Kocha msaidizi wa Sunderland Kevin Ball amekua akishikilia uongozi wa klabu hiyo tangu Di Canio afutwe kazi kutokana na malalamiko ya wachezaji.
Kocha aliyekuwa wa muda Kevin Ball pale Sunderland, pia inaaminika pamoja na kupewa kibarua hicho cha muda alikuwa analilia nafasi hiyo klabuni hapo. Wengine waliokuwa wanahusishwa ni Steve McClaren, Roberto Di Matteo na Tony Pulis.


KUHUSU POYET
July 2006 - Assistant at Swindon with Dennis Wise taking over as manager
October 2006 - Both Poyet and Wise moved to Leeds keeping the same roles
October 2007 - Becomes first team coach at Spurs under Juande Ramos
November 2009 - Takes over as boss at Brighton, winner the League One title in 2011
June 2013 - Sacked as manager of Brighton after a club inquiry
October 2013 - Appointed Sunderland manager

No comments:

Post a Comment