Dakika ya 57 kipindi cha pili Mchezaji wa Newcastle Debuchy anaisawazishia bao Newcastle united baada ya mpira kupigwa na kuwapita mabeki wa Sunderland na hatimaye Debuchy kutokea nyuma na kufunga bao hilo. Dakika ya 84 Fabio Borini anaipachikia bao la pili Sunderland na kufanya 2-1 dhidi ya timu ya Newcastle United. Sunderland ambayo ilikuwa na kiu na ukame wa kushinda na ikiwa inashikilia nafasi ya mkiani inapata ushindi kwenye mtanange huu tena ikiwa ni mechi ya kwanza kushinda tangu msimu huu uanze!!. Ushindi huu wa Sunderland unawaweka nafasi 19 wakiwa na pointi 4 na Newcastle nafasi ile ile ya 10 wakiwa na pointi 11. Crystal Palace wanashikilia nafasi hiyo ya mkiani sasa.
No comments:
Post a Comment