Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, October 28, 2013

CHELSEA 2 v MANCHESTER CITY 1, TORRES AIKWAMISHA CITY DARAJANI STANFORD!! MOURINHO AFURAHIA USHINDI NA KUSHANGILIA

Chelsea wakicheza kwenye uwanja wao Stanford Bridge leo kwenye mchezo wa ligi kuu England, Mchezaji wa Chelsea Andre Schürrle ndie ameifungia bao dakika ya 33 Chelsea baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Torres. Kipindi cha kwanza kilimalizika Chelsea wakiwa juu ya bao 1-0 dhidi ya timu ya Manchester City.Kipindi cha pili dakika 49 Aguero anaisawazishia bao Manchester City baada ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Chelsea.  Late winner: Fernando Torres capitalised on a late defensive slip to give Chelsea a 2-1 winDakika za majeruhi dakika ya 90 Fernando Torres akawafunga bao City baada ya kufanya makosa ya Matija Nastasic kwa kumrudishia kwa kichwa pasi Joe Hart ili adake hatimaye pasi hiyo ikawa tofauti na Torres kufunga bao hilo dakika za lala salama.
Mchezaji wa Manchester City David Silva akimwendesha Eden Hazard wa Chelsea katika kipindi cha kwanza.

Mchezaji wa Chelsea Andre Schurrle akiifungia bao timu yake
Schurrle akituma salamu kwa mashabiki wake darajani ....City hoi!!

Sergio Aguero akishangilia vikali baada ya kuisawazishia bao City kwa kufanya 1-1 kipindi cha pili

Gary Cahill akijaribu kumzuia Sergio Aguero

Andre Schurrle akipongezwa baada ya kuipa bao la kwanza Chelsea Stanford Bridge usiku huu

....Mpaka ndani

Baada ya kutupia nyavuni

Hakunaga!!  Fernando Torres kama kawaida yake na leo kakosa kufunga bao la wazi ...na hapa akijilaumu sana kwa kukosa bao hilo..lakini kipindi cha pili alisahihisha makosa yake.

Majanga!!....ntasomekaje ...? lakini ngoja..!!

Sergio Aguero akiwekwa kati na  Fernando Torres na Ashley Cole

 Fernando Torres akimchomoka  defender Martin Demichelis

Kocha wa  Manchester City  Manuel Pellegrini baada ya kuona mchezaji wake anafanya makosa ya kutoifunga Blues

Ashley Cole na Samir Nasri wakichuana kugombea mpira

David Silva na Eden Hazard  kwenye patashika

Mapema  Chelsea na Manchester City  walisalimiana kabla ya kipute kuanza.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard (Mikel 65), Schurrle (Willian 65), Oscar, Hazard (Eto'o 83), Torres
Substitutes not used: Luiz, Schwarzer, Azpilicueta, Mata
Scorer: Schurrle 32, Torres 90+1
Booked: Lampard, Ramires

Manchester City: Hart, Zabaleta, Demichelis, Nastasic, Clichy, Javi Garcia (Kolarov 80), Fernandinho, Nasri (Jesus Navas 69), Toure, Silva, Aguero (Negredo 86) 
Substitutes not used: Richards, Milner, Dzeko, Pantilimon
Scorer: Aguero 48 
Booked: Zabaleta, Nastasic, Javi Garcia 
Referee: Howard Webb 
Attendance: 41,495

No comments:

Post a Comment