Pages

Tuesday, October 22, 2013

ADNAN JANUZAJ KIKOSINI KESHO DHIDI YA SOCIADAD.

  • Venue: Old Trafford
  • Date: Wednesday, 23 October
  • Kick-off: 19:45 BST
Meneja wa Manchester United David Moyes ana wasiwasi has juu ya kuwatumia walinzi Nemanja Vidic na Rio Ferdinand  kuelekea kukutana dhidi ya Real Sociedad.
Walinzi hao wa kati walikosekana katika mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi yaSouthamtom mwishoni mwa juma kufuatia kukumbwa na maumivu.
Kiungo Tom Cleverley naye amekuwa katika maumivu na hii leo amekosekana katika mazoezi.
Mshambuliaji Danny Welbeck pia alikosekana katika mazoezi ya mwisho ya United kuelekea katika mtanange huo wa kundi A.
United inakuwa na ahueni ya kupatikana na kiungo wa kimataifa wa Belgium Adnan Januzaj, ambaye ameongezwa katika kikosi cha Champions League akiwa kama kijana aliyekulia nchini England na huenda ikawa ni mchezo wake wa kwanza dhidi ya Wahispania wa Sociadad. 
 
Moyes amenukuliwa akisema
"Sasa anapatikana katika ligi ya mabingwa ambao umri unamruhusu.
Ni kijana safi mwenye maendeleo mazuri na ni mtu ambaye atakuja kucheza nafasi kubwa hapo baadaye ndani ya  Manchester United.

No comments:

Post a Comment