MSHAMBULIAJI
nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi na baba yake wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani nchini Hispania kujibu mashitaka ya ukwepaji kodi
yanayowakabili. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa
miaka 26 ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara nne
mfululizo na baba yake Jorge Messi wanatuhumiwa na mamlaka kwa kukwepa
kodi inayokadiriwa kufikia euro milioni nne.
Wote wawili wanahisiwa kutumia kampuni
za nje kuuza haki za kutumia picha ya Messi kinyume cha utaratibu. Messi
na baba yake walikana tuhuma tuhuma hizo ambazo zilifanyika katika
kipindi cha mwaka 2007 na 2009.
Watu wengi walisonga kumuona Messiwengine wakitaka kumpiga picha
Baba Wa Messi, Jorge alipofika kituoni Gava
No comments:
Post a Comment