Pages

Saturday, September 28, 2013

MANCHESTER UNITED YACHAPWA NA WEST BROMWICH ALBION 2-1 KWENYE ENGLISH PREMIER LEAGUE, DAVID MOYES HOI KWA KICHAPO

 West Albion ndio walioanza kufunga bao la kuongoza kipindi cha pili dakika ya 54 Baada ya Morgan Amalfitano wa West Albion kukatiza na kuwapiga chenga mabeki wa United na kuachia shuti kali.Baada ya dakika 3 kupita mchezaji matata wa United Wayne Rooney akaachia frii kiki kwa shuti kali ambalo limeingia moja kwa moja nyavuni. Dakika ya 67 Manchester United wakafungwa bao la pili na Saido Berahino kwa shuti kali. Mpira umemaliza dakika 90 huku kocha Moyes akiwa anajiuliza maswali mazito sana akiwa kwenye uwanja wake Old Trafford. Kipigo hiki cha Kwa Manchester United kinawaporomosha chini zaidi huku West Bromwich wakipanda juu Marouane Fellaini na Robin van Persie wa Manchester United wote wameanzia benchi mechi hiiShinji Kagawa wa Manchester United akipambana na Scott Sinclair wa West Bromwich AlbionJavier "Chicharito" Hernandez wa Manchester United  akipambana na Gareth McAuley kuliaMarouane Fellaini hoi baada ya Man United kufungwa bao la pili akiwa bado yupo benchiPhil Jones wa Manchester United kwenye kasi na mpira akikabwa na Victor Anichebe wa West Bromwich Rio Ferdinand akimkaba vilivyo mchezaji mdogo wa miaka 20 Saido Berahino wa West BromwichRooney kushoto nae akikabwa na Saido Berahino

Wayne Rooney akipongezwa na wenzake baada ya kusawazisha bao dakika ya 5.
Bao la Saido Berahino, limewapa West Brom ushindi wao wa kwanza dhidi ya Manchester United Uwanjani Old Trafford tangu Mwaka 1978 kwa kushinda Bao 2-1.
Bao zote zilifungwa Kipindi cha Pili na WBA walitangulia kufunga kupitia Morgan Amalfitano na Wayne Rooney kusawazisha Dakika 3 baadae.
Marouane Fellaini aliweza kuisawazishia Man United lakini Bao hilo lilikatawaliwa kwa Ofsaidi na kuifanya Man United iwe imeanza vibaya Ligi kupita wakati wowote tangu Msimu wa 1989/90.
Shinji Kagawa wa Manchester Unitedakigombania mpira na Youssuf Mulumbu kipindi cha kwanzaMorgan Amalfitano akimfunga bao la kwanza kipa David de GeaUnited Hoi baada ya kufungwa bao hilo la kwanza kipindi cha pili dakika ya 54Baadae kidogo dakika ya 57 Rooney alifunga bao na kusawazisha na hapa alikuwa anapongezwa na wachezaji wenzake.Furaha kwa United hapa..Saido Berahino akachafua hali ya hewa Old Trafford akawashona bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya United kwenye uwanja wao wa nyumbani.Saido Berahino akipongezwa..Wachezaji wa United wakijiuliza hapa kuna nini!!! Rooney nae...hoi..David Moyes..akishangaa dakika zikiyoyoma!!David Moyes akiwa anajiuliza maswali mazito kwenye uwanja wa Old Trafford Rooney ...hoi nae...

David de Gea kipa wa United kilio baada ya mtanange!!!

No comments:

Post a Comment