Pages

Wednesday, September 4, 2013

LUKAKU APELEKWA EVERTON KWA MKOPO






LONDON, England
KLABU ya Chelsea imethibitisha kwamba imeamua kumpeleka kwa mkopo straika wake aliyekosa penati katika mechi ya Super Cup dhidi ya Bayern Munich, Romelu Lukaku, kwenye kikosi cha Everton kwa msimu mzima.

Mtandao wa Goal.com ulibaini juzi usiku kuwa straika huyo mwenye umri wa miaka 20, raia wa Ubelgiji, amekubali kutua ndani ya dimba la Goodison Park, na alikuwa Merseyside hadi juzi usiku, muda mchache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamisho wake.

Lukaku amekwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi cha Roberto Martinez, baada ya kiungo mshambuliaji wa timu, Marouane Fellaini, kutimkia Manchester United na Victor Anichebe kwenda West Brom.

"Romelu Lukaku ataendelea na msimu wa pili wa Ligi Kuu ya England akiwa nje kwa mkopo na safari hii atatimkia kwenye kikosi cha Everton," Chelsea ilitoa taarifa kupitia mtandao wake juzi.

"Kupelekwa kwake Goodison Park kunafuatia mafanikio mazuri aliyoyapata msimu uliopita, alipokuwa kwenye kikosi cha West Bromwich Albion ambako alicheza mechi 38 na kufunga mabao 17, na kuwa mfungaji bora zaidi mwenye umri mdogo kwenye Ligi Kuu ya England tangu Michael Owen alipofanya hivyo msimu wa 1998/99."

Lukaku mwenyewe alithibitisha mapema kupitia mtandao wake wa Twitter akisema: "Nimesaini Everton kwa mkopo wa msimu mpya."

No comments:

Post a Comment