LONDON, England
STRAIKA wa Tottenham Hotspur, Gylfi Sigurdsson (24),
alishindwa kutua Sunderland akitokea Spurs kutokana na sakata la uhamisho wa Gareth
Bale kwenda Real Madrid, inasemekana Sigurdsson ambaye alifunga bao la Spurs
kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea, alitakiwa na Sunderland na jamaa
walikuwa tayari kutoa pauni milioni 10 kwa ajili yake, lakini kampuni yake ya
uwakala ya Stellar Group ilikuwa imeelekeza nguvu zake zote kufanikisha
uhamisho wa Bale na kumsahau yeye.
@@@@
Everton
wapania kumbakiza Barry
LIVERPOOL, England
EVERTON wanataka kumpa mkataba wa kudumu, Gareth Barry (32),
anayeichezea klabu hiyo kwa sasa kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester
City, inasemekana kocha wa miamba hiyo ya Goodison Park, Roberto Martinez,
ameridhishwa na kiwango cha nyota anayepokea kiasi cha pauni 120,000 (sh
milioni 304.363) kwa wiki na anataka kumbakiza baada ya mkataba wake wa mkopo
kuisha.
@@@@
Fletcher
kurudi uwanjani Oktoba
MANCHESTER, England
KIUNGO wa Manchester United, Darren Fletcher (29)
anatarajiwa kurudi uwanjani Oktoba, mwaka huu baada ya kukaa benchi kwa muda
mrefu akisumbuliwa na majeruhi, bado haijafahamika siku rasmi ambayo Fletcher
atarudi uwanjani, lakini madaktari wa Man Utd wanaamini itakuwa Oktoba, hii ni
baada ya kukaa benchi tangu Januari, huku katika kipindi cha miaka miwili
akicheza mechi saba tu, kutokana na matatizo ya kiafya.
@@@@
Mustakabali
wa Terry mikononi kwa Mourinho
LONDON, England
MUSTAKABALI wa John Terry (32), katika klabu ya Chelsea, uko
mikononi kwa kocha wake, Jose Mourinho, ambaye ndiye ameshika rungu la kuamua
kumuongeza mkataba au kumuacha aende zake pindi mkataba wake wa sasa
utakapomalizika. Zamani Mkurugenzi wa Ufundi, Michael Emenalo na Bodi ya klabu
ndiyo walikuwa na sauti ya kuamua, lakini sasa hivi Mourinho ndiye mwenye sauti
ya mwisho kwenye ishu ya Terry na Frank Lampard.
No comments:
Post a Comment