Pages

Wednesday, September 4, 2013

BAADA YA KUSHIKILIA USUKANI WA LIGI KUU, JKT RUVU YAANZA TAMBO



KOCHA Msaidizi wa JKT Ruvu, Azish Kondo, amesema hakuna timu itakayowang’oa kileleni msimu huu, baada ya kufanikiwa kuwaondoa Yanga waliokuwa wakishikilia nafasi hiyo.

Akifafanua kauli yake hiyo, Kondo alisema imekuwa kawaida kwa kikosi hicho kuongoza ligi, lakini baada ya muda inashushwa na Simba, Yanga, Azam na Mtibwa Sugar, jambo ambalo msimu huu wamelikataa kuona likitokea.

Alisema sababu zilizokuwa zinawafanya washushwe kileleni msimu uliomalizika ni baadhi ya wachezaji wao kwenda katika mafunzo ya kijeshi na kuwafanya kuchoka,  lakini msimu huu nyota wao wote tegemeo wamerejea na wapo vizuri.

“Kwa sasa wachezaji wetu wapo, hivyo tunajihakikishia kufanya mambo makubwa msimu huu, tutang’ang’ania nafasi hiyo hadi mwisho wa ligi kwa sababu nia yetu ni kutaka kupata ubingwa,” alisema.

Kikosi hicho kinaongoza ligi hiyo kikiwa na pointi 6, baada ya kushuka dimbani mechi mbili na kufanikiwa kushinda zote, hali iliyowafanya kuwashusha waliokuwa wanaongoza ligi hiyo, Yanga, ambayo sasa inashikilia nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment