Pages

Sunday, August 25, 2013

TOTTENHAM YAIFUNGA SWANSEA CITY 1-0, ROBERTO SOLDADO AFUNGA PENATI NA KUIPA USHINDI SPURS



TOTTENHAM 1 vs SWANSEA 0
BAO la pekee na la penati ya Dakika ya 58 iliyopigwa na kufungwa na Roberto Soldado, likiwa ni Goli lake la 4 kwa Mechi 3 katika Timu yake mpya, leo limewapa ushindi wa Bao 1-0 Tottenham waliokuwa wakicheza Nyumbani White Hart Lane dhidi ya Swansea City katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Jonjo Shelvey kumchezea rafu Andros Townsend.
Huu ni ushindi wa pili kwenye Ligi kwa Tottenham kufuatia kuifunga Cardiff City Bao 1-0 katika Mechi ya kwanza na hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Swansea baada ya kuchapwa Bao 4-1 na Man United katika Mechi ya ufunguzi.

Roberto Soldado akifunga penati yake ya pili leo na kuipa ushindi Spurs
Soldado akishangilia hapa baada ya kumfunga kipa Michel Vorm

Moussa Dembele akichuana na Jose Canas
 VIKOSI:
Tottenahm: Lloris 7; Walker 5, Dawson 7, Vertonghen 7, Rose 6; Capoue 6; Townsend 7 (Sandro 87), Paulinho 6, Dembele 5 (Sigurdsson 63, 5), Chadli 5; Soldado 6 (Defoe 79).
Subs not used: Kaboul, Naughton, Friedel, Carroll.
Booked: Soldado.
Goals: Soldado (pen) 58.
Swansea: Vorm 8; Rangel 6, Flores 7, Williams 6, Davies 6; Shelvey 5 (Bony 68, 4), Canas 6, De Guzman 5; Hernandez 5, Michu 5, Routledge 5 (Pozuelo 58, 5).
Subs not used: Tremmel, Amat, Britton, Lamah, Richards.
Booked: Davies, Vorm, Michu, Williams.
Referee: T Neil Swarbrick

No comments:

Post a Comment