Pages

Thursday, August 29, 2013

SUPERCOPA DE ESPAÑA: BAO LA UGENINI LAWALINDA BARCA, WATWAA KOMBE MARA YA 11


Champions: Barcelona celebrated a record eleventh Spanish Super Cup against Atletico MadridJANA USIKU, ndani ya Uwanja wa Nyumbani Nou Camp, Mabingwa wa Spain Barcelona wamefanikiwa kutwaa Supercopa De Espana baada ya kutoka 0-0 na Atletico Madrid na wao kutwaa Kombe hilo kwa vile walitoka sare 1-1 Wiki iliyopita huko Estadio Vicente Calderon na hivyo kufuzu kwa Bao la Ugenini. Katika Mechi hiyo Kipa wa Barca Victor Valdes alionyesha umahiri mkubwa kwa kuokoa Goli za wazi za Arda Turan na David Villa. Atletico walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Filipe Luis kupewa Kadi Nyekundu na Mechi hii kwisha kwa Barca kupewa Penati ya Dakika ya 89 kufuatia Pedro kuangushwa na Miranda na Lionel Messi akapiga na Mpira kupiga posti. Akilalamikia Penati hiyo, Mchezaji wa Atletico Turan ambae alikuwa tayari yupo Benchi baada ya kubadilishwa alipewa Kadi Nyekundu na Refa.
Luis alipewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Dani Alves katika Dakika ya 89. Neymar, ambae alianza Mechi hii, alishindwa kushirikiana vyema na Messi. Hili ni Taji la 16 kwa Barca katika Miaka minne na la kwanza kwa Kocha mpya Gerardo ‘Tata’ Martino ambae alisema Taji hilo ni la Kocha aliemtangulia ambae ni Mgonjwa, Tito Vilanova. Alisema: “Nimeshinda Taji hili kwa ajili ya mambo yalivyotokea. Kombe hili ni la Wachezaji, Tito Vilanova na Wasaidizi wa Makocha!”
Mshindi: Bao la Neymar katika mechi ya kwanza limempa taji la kwanza Barcelona

Neymar (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake, Dani Alves na Super Cup ya Hispania

Mabingwa: Barcelona wamesherehekea rekodi ya kutwaa Super Cup ya 11 Hispania dhidi ya Atletico Madrid

Mchuano: Lionel Messi (kulia) akipambana na David Villa
Mkwaju wa penati

Juanfran wa Atletico Madrid (kushoto) akigombea mpira wa juu na Neymar wa Barcelona (kulia)

Anapaa: Cesc Fabregas akiwatoka Joao Miranda na Mario Suarez (kulia)

Mchezaji mwenzake wa zamani: Gerard Pique (kulia) akipambana na mshambuliaji wa Atletico, David Villa

Bao la wazi: Nyota wa Barcelona, Neymar akisikitika baada ya kukosa bao

Anavuta jezi: Arda Turan wa Atletico akimvuta jezi Messi

Barcelona

Atlético Madrid

Possession

78%

22%

Total Shots

8

8

Shots on Target

1

3

Pass Accuracy

90%

69%

Fouls

9

27

Offsides

0

2

Yellow Cards

3

3

Red Cards

0

2

No comments:

Post a Comment