Pages

Friday, August 30, 2013

RIBERY MCHEZAJI BORA ULAYA



MONACO, Ufaransa
WINGA wa Bayern Munich Franck Ribéry ameibuka kidedea katika tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa mwaka 2013 na kuwabwaga Lionel Messi na Cristiano Ronaldo aliokuwa akichuana nao kwenye kinyang’anyiro hicho.

Katika ghafla hiyo ambayo ilifanyika jijini Monaco, Ufaransa upigaji wa kura za mchezaji bora ulifanyika ‘Live’ na Ribery kuwafunika wawili hao ambao wamekuwa wakitawala soka katika miaka ya karibuni.

Ronaldo hakutokea katika hafla hiyo, ambapo Ribery baada ya kutangazwa mshindi aliwashukuru wachezaji wenzake wa Bayern na familia yake kwa sapoti waliyompa.

Katika hatua nyingine mbali na hafla hiyo pia ilishuhudia upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa 2013-14.

KUNDI A
Manchester United
Shakhtar Donetsk
Bayer Leverkusen
Real Sociedad

KUNDI B
Real Madrid
Juventus
Galatasaray
Kobenhavn

KUNDI C
Benfica
PSG
Olympiacos
Anderlecht

KUNDI D
Bayern Munich
CSKA Moscow
Manchester City
Viktoria Plzen 

KUNDI E
Chelsea
Schalke 04
FC Basel
Steaua Bucharest 

KUNDI F
Arsenal
Olympic Marseille
Borussia Dortmund
Napoli

KUNDI G
Porto
Atlético Madrid
Zenit st-Petersburg
Austria Wien

KUNDI H
Barcelona
AC Milan
Ajax
Celtic

No comments:

Post a Comment