Pages

Thursday, August 29, 2013

MOROCCO: BOBAN NA NYOSO WATAISAIDIA COASTAL UNIONN



KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Hemed Morocco, amesema kiwango kinachoonyeshwa na wachezaji wa zamani wa Simba kitasaidia kikosi chake  kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Morocco aliwataja wachezaji hao kuwa ni Haruna Moshi 'Boban (kiungo), Juma Nyoso (beki) na Uhuru Seleman (mshambuliaji).
Aliwaelezea nyota hao kwamba wamekuwa chachu ya ushindani wa namba kwenye kikosi hicho.

"Kiwango cha wachezaji hao ni cha hali ya juu, naamini watasaidia timu yetu kufanya vema katika ligi msimu huu," alisema.

Alisema hana maana kwamba wachezaji wengine hawana uwezo, ila kila mchezaji ana nafasi yake katika timu hiyo.

Pia alisema kuwa pambano lao dhidi ya Yanga lilikuwa gumu, lakini mapungufu ambayo yalijitokeza watayafanyiwa kazi ili yasijirudie katika michezo ya mbele.

"Kwa sasa nguvu zetu tunaelekeza katika mechi ya mbele ili kuhakikisha malengo yetu yanatimia.

No comments:

Post a Comment