Mchuano wa kufuzu kwa
fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kati ya Senegal na Uganda unatarajiwa
kupigwa nchini Morocco tarehe 7 ya mwezi Septemba mwaka huu. Kwa mujibu wa
taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Shirikisho la soka duniani FIFA, mechi
hiyo itafanyika katika mji mkuu wa Morocco, Marrakesh.
Mataifa hayo yapo
katika kundi J, na Senegal wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama tisa,ikiwa ni
alama moja mbele ya Uganda wenye pointi nane.
Senegal walizuiliwa kucheza
katika viwanja vya nyumbani baada ya ghasia zilizozuka wakati wa mechi ya kufuzu
kwa michuano ya AFCON ya mwaka 2013 dhidi ya Ivory Coast. ![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vySPTWdna0_gc1QgbnlIz30Nbyoq5G1S6ZVBz07BBPisydqEjzZPN8UPfGfpxHDD6DGKuJSviJH0X4BvfuNasMBRGnw0QIG3xWe4d5kMzIYkDlRyXpfWj0qiKI07p27M5FcXSE1q_LDJa3EiulBLRofOmQD36fmxU=s0-d)
Uganda wanahitaji ushindi katika mechi hiyo ili waweze kuingia katika raundi ya mwisho ya michuano ya kufuzu kwa timu za Afrika kabla ya kuelekea Brazili hapo mwakani.
Uganda wanahitaji ushindi katika mechi hiyo ili waweze kuingia katika raundi ya mwisho ya michuano ya kufuzu kwa timu za Afrika kabla ya kuelekea Brazili hapo mwakani.
No comments:
Post a Comment