Pages

Monday, August 19, 2013

MASHETANI WEKUNDU WAFUNGUA MSIMU KWA KUGAWA KICHAPO MBELE YA KOCHA WAO MPYA DAVID MOYES KWA KUIFUNGA SWANSEA 4-1

MABINGWA watetezi wa taji la ligi kuu nchini England, Mashetani Wekundu, Manchester United, wametoa kipondo cha mbwa mwizi kwa klabu ya Swensea City cha mabao 4-1.
Wayne Rooney aliingia kipindi cha pili, lakini ni Robin van Persie na Danny Welbeck ambao wamempa mwanzo mzuri zaidi kocha wao David Moyes katika maisha yake klabuni Manchester United.

ARV aliandika bao la kwanza katika dakika ya 34, dakika ya 36 Welbeck aliandika bao la tatu, katika dakika ya 72 ARV aliandika kimiani bao la tatu akipokea pasi nzuri kutoka kwa Wayne Mark Rooney. 

Na sherehe ya mabao ilihitimishwa na Welbeck katika dakika 90 akipokea pasi murua kutoka kwa Rooney ambaye ni gumzo kubwa katika usajili wa majira haya ya kiangazi. 

Swansea walipata bao la kuwadanganyishia mashabiki wao kuwa walikaza lakini ndio basi tena katika dakika 82 kupitia kwa Bony Wilfried akipokea pasi nzuri kutoka kwa Pablo Hernande.
Robin van Persie akitupia bao la tatuRobin van Persie akishangilia huku Patrice Evra akimpongeza kwa kumrukia na kubebwa juu juuDanny Welbeck akipongezwa baada ya kufunga bao la piliDanny Welbeck  akikabwa na mtu mbili Leon Britton na mchezaji mwingine nyumaVan Persie akifunga bao la kwanza hapa.Danny Welbeck ndiye aliyekuwa mwiba kwenye mtanange huu akifatiwa na Rvp ambao wote wamefunga bao mbili mbili
Michael Carrick akikaba
Veteran Giggs naye akiendesha hapaMajanaga!!Wayne Rooney ameanzia benchi mechi hii..
VIKOSI:
Swansea: (4-5-1) Vorm 6; Rangel 6, Flores 6, Williams 5, Davies 6; Britton 6 (Bony 46, 6),Canas 5 (Ki 76, 6), Shelvey 7, Dyer 6, Routledge 6 (Hernandez 46, 6); Michu 6.
Subs not used: Tremmel, Amat, Pozuelo, Taylor.
Booked: Canas.
Goal: Bony 82.
Manchester United: (4-4-2) De Gea 6; Jones 6, Ferdinand 6, Vidic 6, Evra 6; Valencia 6, Carrick 7, Cleverley 7, Giggs 6 (Rooney 61 6); Welbeck 8, Van Persie 8 (Anderson 86).
Subs not used: Lindegaard, Smalling, Fabio, Kagawa, Zaha.
Booked: Carrick, Cleverley, Valencia.
Goals: Van Persie 34, 72, Welbeck 36, 90.
Ref: Dowd.
Att: 20,733.

No comments:

Post a Comment