Pages

Tuesday, August 27, 2013

MANCHESTER UNITED NA CHELSEA ZATOKA SARE 0-0 MBWEMBWE ZA JOSE ZAGONGA UKUTA OLD TRAFORD


MANCHESTER UNITED 0 vs CHELSEA 0
Kipindi cha kwanza kilimalizika nguvu sawa ya bila kufungana, huku Chelsea mchezaji wake Oscar akijaribu na kuonesha nia ya kuipachikia bao Chelsea baada ya kujaribu mara kadhaa akiwa nje ya box. Wao Manchester United wakitawala dakika kama 30 uwanjani na wakikosa nafasi kadhaa. 
 Man United ndiyo waliopata nafasi nzuri zaidi za ushindi na hata ‘kunyimwa Penati’ ya Kipindi cha Pili pale shuti la Tom Cleverley lilipomgonga mkononi Frank Lampard na Refa Martin Atkinson kupeta.
Rooney akicheza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha kwanza tangu msimu huu mpya uwanze ameonesha kiwango cha hali ya juu akishirikiana na Van Persie. Kipindi cha pili pia kimemalizika bila ya kufunga huku timu ya Manchester United ikicheza kwa kujiamini na kuwapa kashkaji wachezaji wa Chelsea na kwa kuwakaba kisawasawa na United kupoteza nafasi za kufunga katika kipindi hicho cha pili. Mpaka dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyoziona nyavu za mwenzake. 
Hii ndio Sare ya kwanza ya Man United ya 0-0 Uwanjani Old Trafford tangu Mei 2009 walipotoka Droo ya 0-0 na Arsenal na kati yake zimepita Mechi 77 za Ligi.
Wayne Rooney, Mchezaji ambae katika Wiki za hivi karibuni mara mbili alitolewa Ofa za kununuliwa na Chelsea, alicheza kwa bidii mno, kung’ara na kukosa nafasi kadhaa ambayo mojawapo nzuri iliokolewa na Kipa Petr Cech na kuchacharika huko kuliwafanya Mashabiki wa Man United wapige mayowe kumshangilia: “Rooney, Rooney!”
Nafasi murua kwa Chelsea ni shuti la mbali la Beki Gary Cahil.
Sare hii inawapa alama moja moja kila timu huku Chelsea wakiwa juu kileleni na pointi zao 7 na michezo 3 na Manchester United wakiwa na pointi 4 michezo miwili tu. Majanga kwa Patrice Evra baada ya kuumiwa shingo na mwenzake wakati wanaruka juu kugombania mpira
Koha Moyes wa United uwanjani kwa mara ya kwanza akicheza mechi ya nyumbani ligi kuu tangu atue Klabuni hapo na hii ikiwa ni mechi yake kwanza kucheza na Chelsea ikiongozwa Jose Mourihno, wote wakiwa ni makocha wapya!!Rooney akionesha kiwango safi leo hiiWelbeck akituliza mpira kwa makini mbele ya Branislav Ivanovic wa Blues.Van Persie akikabwa na mtu mbili hapa..Kama haitoshi na makocha wengine walikuwepo!!! Everton manager Roberto Martinez na Man City boss Manuel Pellegrini...uendi popote!!....tulia!!
Mapema kabla ya mechi kuanza walianza kumwombea mchezaji wa zamani wa  Manchester United  na trainer Jack Crompton.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia (Young 67), Cleverley, Carrick, Welbeck (Giggs 78), Rooney, Van Persie.
Subs: Anderson, Smalling, Lindegaard, Kagawa, Buttner.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne (Torres 60), Oscar, Hazard (Azpilicueta 93), Schurrle.
Subs: Essien, Mikel, Lukaku, Schwarzer, Mata.
Booked: De Bruyne, Torres.

No comments:

Post a Comment