Pages

Tuesday, August 13, 2013

KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI LEO


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inamekutana jana Agosti 13 mwaka huu na leo  kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya kwanza ya usajili imeshamalizika wakati hatua ya pili ya usajili inaanza leo Agosti 14 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania.

Hivyo, dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment