Pages

Tuesday, August 13, 2013

KAMATI KUTANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF

Mchakato wa uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa leo Agosti 13 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Agosti 11 mwaka huu, na ilikutana tena Agosti 12 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo.

Mbali ya Mbwezeleni, wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara.

No comments:

Post a Comment