Pages

Friday, August 30, 2013

ETO'O KULETA MAPINDUZI YALIYOWASHINDA TORRES NA BA




KOCHA Jose Mourinho,  amefanya uamuzi wa kumsajili mshambuliaji Mcameroon, Samwel Etoo kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala, baada ya jaribio la kumnasa Wayne Rooney kutoka Manchester United kushindikana.
Pengine watu wanajiuliza je, Mourinho hasa anahitaji nini kwani anawashambuliaji mahiri kama vile Fernando Torres, Demba Ba Romelu Lukaku?
Hili ni swali gumu lakini ni la msingi sana, kwani wote ni washambuliaji na sasa kufika kwa Eto’o kutaifanya Chelsea kuwa na washambuliaji wanne katika namba moja.
Jibu ya swali hili ni rahisi kwa Mourinho, pamoja na kwamba Torres na Lukaku ni wafungaji wazuri, Ba ni mpiganaji na mfungaji pia lakini kilichomvuta zaidi Mourinho kumsaka Rooney na hata kumnasa Eto’o ni kutafuta mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufunga, kukaba na kutengeneza nafasi kwa wengine.

Ni wazi kwamba, Mourinho aliwasoma washambuliaji wake wote watatu na kuona kwamba kuna upungufu ndiyo maana amehitaji huduma ya Eto’o kwenye kikosi chake ili kuwa na mbadala wa Torres, Demba Ba.
Kwa aina ya ufundishaji ya kocha huyo kutoka Ureno, isingekuwa rahisi kumtumia mtu kama Torres kwenye kikosi cha kwanza hasa katika mechi ngumu, kwani anahitaji washambuliaji wanaoweza kujipanga na kupanga wenzao na wenye uwezo wa kutengeneza nafasi zao binafsi na kuwatengenezea wengine jambo ambalo Etoo ni mtaalamu zaidi ya Demba na Torres.

Lukaku bado hajaaminiwa sana kushika mikoba ndani ya Stanford Bridge, hii inamuweka pembeni katika vita ya namba ingawa pia suala la uzoefu huwezi kumlinganisha na Etoo.
Msenegal Ba aliifungia Chelsea mabao mawili kwenye ligi  baada ya kununuliwa katika msimu wa dirisha dogo, huku Mhispania akizidi kupoteza makali yake ya ufungaji kama alivyokuwa Liverpool.
Wengi wameshapoteza imani na Torres, kwa sasa si mmoja wa washambuliaji wenye madhara tena kama ambayo ilikuwa ikifahamika.

Torres aliwika sana akiwa Liverpool, iliyokuwa na aina yake ya uchezaji huku Xabi Alonso akipewa jukumu ya kummegea na kumtengea mapande mazuri yaliyomuwezesha kucheka na nyavu mara kwa mara.
Wakati Demba Ba akishangaika kufuta ukame wa mabao uliomkumba tangu Januari, Torres ameshindwa kufikia matarajio ya wadau wa Stamford Bridge na Lukaku bado kinda ambaye anatakiwa kuanzia benchi.
Mourinho amekosa mfungaji hasa wa mabao licha ya kuwa na wapishi mahiri na viungo imara, amefanya uamuzi mgumu kumchukua Etoo, mtu anayemfahamu vyema kwa kuwa alikuwa naye katika kikosi kilichotwaa Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Inter Milan ya Italia.

Pengine Etoo anaweza asiwe suluhisho la muda mrefu kwa Chelsea, kutokana na umri kuanza kumkimbia, lakini mchezaji huyo aliyetwaa klabu bingwa Ulaya mara tatu ataleta faraja darajani.

No comments:

Post a Comment