Pages

Thursday, August 15, 2013

ENGLAND YAIFUNGA SCOTLAND MABAO 3 - 2. LAMBERT AIPA USHINDI ENGLAND!

Mechi hii ya Kirafiki ikichezwa bila Kiungo Michael Carrick ambae ni Kiungo wa Manchester United mwenye Miaka 32, amelazimika kujiondoa baada ya Jicho lake moja kupata ugonjwa. England usiku huu wakicheza na Mahasimu wao wakubwa Scotland ambao hawajakutana nao tangu Novemba 1999. Scotland ndio walianza kuziona nyavu za England kupitia mchezaji wao James Morrison dakika ya 11. Baadae dakika ya 29 Walcott akapenyeza kwenye ngome ya Scotland na kuwapita mabeki na kufunga bao safi. Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinaisha timu zote zilikuwa zinalingana zikiwa na bao 1-1.
Kipindi cha pili dakika ya 50 mchezaji wa Scotland Miller akawapatia bao na kufanya 2-1. England wakaongeza mashambulizi na kuweza kusawazisha bao hilo dakika tatu mbele mchezaji anayeichezea Manchester United Welbeck dakika ya 53 akasawazisha na kufanya 2-2. Dakika ya 70 mchezaji Lambert aliyeingia kipindi cha pili anaunganisha pasi safi kwa kichwa na kuipatia bao la 3 na la ushindi England dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Scotland.
Mechi  hii ya England v Scotland ni sehemu ya Sherehe za FA, Chama cha Soka England kusheherekea Miaka 150 ya uhai wake na Mechi hii itakuwa ya 111 kati ya Mataifa hayo, ya kwanza ilikuwa Mwaka 1872 na baada ya hapo walikutana kila Mwaka hadi 1989.
Mashabiki wa Scotland maarufu kama ‘Tartan Army’wakitokelezea.......James Morrison akishangilia baada ya kuipachikia bao timu yake na hapa akiwa na wenzake wakimpongezaWachezaji wa Scotland wakiwa kwenye furaha baada ya kupata bao lao hapaJames Morrison (kulia) akiachia shuti kali ambalo limepenyeza hadi nyavuni na kufanya 1-0 dhidi ya England usiku huu.James Morrison (kushoto) akizionja nyavuMchezaji wa Scotland Robert Snodgrass akijaribu na yeye kuachia nduki hapa kwenye kipindi cha kwanzaWayne Rooney kwenye patashika na Russell Martin wa ScotlandStaa wa Arsenal Jack Wilshere kulia nae hapa akionekana kuumiliki vyema mpira...Walcott akapenyeza kwenye ngome ya Scotland na kuwapita mabeki na kufunga bao safi. Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinaisha timu zote zilikuwa zinalingana zikiwa na bao 1-1.Leighton Baines na  Alan Hutton wa Scotland wakichuanaTheo Walcott akishangilia pamoja na Tom Cleverley baada ya kusawazisha....Theo Walcott akitupiaWelbeck akifurahia hapa na kupeta baada ya kusawazisha bao dakika ya 53 kwa pasi safi ya kichwaWelbeck
VIKOSI:
England:
Hart, Walker, Cahill, Jagielka, Baines, Cleverley (Milner 67), Gerrard (Oxlade-Chamberlain 62), Wilshere (Lampard 46), Walcott, Rooney (Lambert 67), Welbeck.
Subs: Foster, Johnson, Cole, Jones, Smalling, Defoe, Zaha, Ruddy.
Goal: Walcott 29, Welbeck 53, Lambert 70.
Booked: Walker, Walcott.


Scotland: McGregor, Hutton, Martin, Hanley, Whittaker, Snodgrass (Conway 67), Morrison, Brown, Forrest (Mulgrew 67), Maloney, Miller.
Subs: Gilks, McArthur, Naismith, Burke, Adam, Webster, Rhodes, Bannan, Griffiths, Mackay-Steven, Dorrans, Boyd, Greer, Hammell, Marshall.
Goal: Morrison 11, Miller 50.
Booked: Snodgrass.

Referee: Felix Brych (Germany)

No comments:

Post a Comment