Pages

Saturday, August 31, 2013

CHEKA AMCHAKAZA MMAREKANI DIAMOND JUBILEE NA KUCHUKUA UBINGWA WA WBF, UZITO WA KATI


Bondia Francis Cheka na Phil Wiliams wakirushiana makonde

Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akimvisha Cheka mkanda kulia ni Rais wa WBF


Cheka akimnong'oneza jambbo Phil Williams baada ya pambano kumalizika

Mashali (kushoto) akipambana na Mada Maugo (kulia)

Phil Williams hapa kapata konde hadi shingo ikageukia nyuma
 BONDIA Cheka Francis jana usiku aliwatoa kimasomaso watanzania baada ya kumpiga bondia Phil Williams toka Marekani lililochezwa Diamond Jubilee, Dar es salaam.

Katika pambano hilo lililochezeshwa na refa kutoka Afrika Kusini, Drake Ribbinck, mabondia hao walianza kwa kusomana raundi ya kwanza wakitupiana makonde kwa tahadhari na katika raundi ya pili, kila mmoja alitaka kuhakikisha kile alichogundua kwa mpinzani wake kabla ya kazi kuanza raundi ya Tatu.

Cheka aling’ara katika raundi ya tatu na ya nne na Mmarekani akaibuka Raundi ya tano na kuanza kuonyesha upinzani. Raundi ya sita Mmarekani aliongeza kasi ya urushaji makonde ingawa Williams alianguka kwa kuteleza na kuinuka kuendelea na pambano.

Raundi ya 10 mabondia hao waliendelea kutupiana makonde kwa zamu, lakini raundi ya 11 na 12 pamoja na Williams kusimama imara kutafuta ushindi wa Knockout (KO), lakini SMG alikuwa makini katika kukwepa na kurusha ngumi za kudonoa kichwani kwa mpinzani wake.

Na kwa sababu hiyo haikushangaza baada ya pambano, bondia mwenye maskani yake Morogoro kutangazwa bingwa mpya wa WBF.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara aliyekuwa mgeni rasmi alimvisha taji Cheka ingawa ulingo ulivamiwa na mashabiki waliopagawa na ushindi wa bondia huyo.

Katika mapambano ya utangulizi, Thomas Mashali alimshinda kwa pointi Mada Maugo, wakati Alphonce Mchumia Tumbo alimshinda kwa Technincal Knockout (TKO), baada ya wasaidizi wake kurusha taulo raundi ya tano katika pambano la raundi sita.

Hata hivyo, dosari  iliyojitokeza katika usiku huo ni mabondia kugoma kupanda ulingoni hadi kwanza walipwe fedha zao na ilianzia kwa Mchumia Tumbo, ikafuatia kwa Maugo na Mashali na baadaye Cheka.

Bingwa wa zamani wa dunia, bondia wa Afrika Kusini, Francois Botha alilaani hali hiyo na kusema mabondia wanapanda ulingoni kwa ajili ya fedha, hivyo kutokokuwa na uhakika wa malipo yao si sawa.

Alipoulizwa kuhusu malipo yake, Botha aliyewahi kupigwa kwa mbinde na bingwa wa zamani wa dunia, Mmarekani, Mike Tyson alisema yeye amekuja kwa mradi maalum wa kampeni kuzuia Malaria na hana anachodai kwa waandaaji wa pambano hilo.

Miongoni mwa mabondia Wamarekani wengine  ambao aliwahi kupigwa  ni Garvin Crout alipigwa na Mtagwa, mtoto wa Keko Mwanga, Temeke, Dar es Salaam kwa Knockout (KO) Raundi ya kwanza pambano la Raundi nane

No comments:

Post a Comment