Pages

Thursday, August 29, 2013

CAPITAL ONE CUP: DROO YA RAUNDI YA 3, MANCHESTER UNITED vs LIVERPOOL, MABINGWA WATETEZI SWANSEA KUANZA UTETEZI NA BIRMINGHAM



JANA, mara baada ya kukamilika kwa Mechi za Raundi ya Pili, ilifanyika Droo ya Raundi ya Tatu ambayo ilijumuisha Timu za Ligi Kuu England ambazo zipo Ulaya zinakocheza Mashindano ya UEFA na Mabingwa wa England Manchester United wamepangiwa kucheza na Mahasimu wao wakubwa Liverpool Uwanjani Old Trafford.
Mabingwa Watetezi Swansea City wamepangiwa kwenda kucheza Ugenini na Timu ya Daraja la Championship Birmingham.
Mechi zitakazohusisha Timu za Ligi Kuu pekee ni zile za Aston Villa v Tottenham, West Brom v Arsenal, West Ham v Cardiff na Everton v Fulham.
Mechi hiyo ya Man United v Liverpool huenda ikawa ndio Mechi ya kwanza ya Luis Suarez baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 10 kwa kumng’ata Branisla Ivanovic wa Chelsea kwenye Mechi.

DROO YA RAUNDI YA 3
[Mechi kuchezwa Septemba 24 na 25]
Man Utd v Liverpool
Sunderland v Peterborough
West Ham v Cardiff
Man City v Wigan
Burnley v Nottingham Forest
Newcastle v Leeds
Southampton v Bristol City
West Brom v Arsenal
Swindon v Chelsea
Tranmere v Stoke
Watford v Norwich
Aston Villa v Tottenham
Hull v Huddersfield
Leicester v Derby
Birmingham v Swansea
Fulham v Everton

No comments:

Post a Comment