Pages

Friday, August 30, 2013

BESIKTAS YAENGULIA EUROPA LEAGUE BAADA KUSHINDWA RUFANI YAO.


KLABU ya Besiktas ya Uturuki imeshindwa rufani yao waliyokata kupinga kufungiwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kwa kujihusisha na upangaji matokeo ya baadhi ya mechi za ligi.Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS ilitangaza uamuzi wake wa kutupilia mbali rufani iliyokatwa na klabu hiyo hivyo kuendelea na kifungo chao cha mwaka mmoja walichopewa na UEFA na kufanya klabu hiyo kuenguliwa katika michuano ya Europa League msimu huu. Nafasi yake katika hatua ya makundi itachukuliwa na klabu ya Tromso ya Norway pamoja na kuwafunga katika mechi ya mtoano iliyochezwa jana. Klabu ya Fenerbahce nayo nafasi yake itachukuliwa na klabu ya APOEL ya Cyprus baada ya wao pia kushindwa katika rufani yao waliyopeleka CAS.

No comments:

Post a Comment