Pages

Friday, July 5, 2013

WAYNE ROONEY ATAKIWA KUANDIKA BARUA ENDAPO KWELI ANATAKA KUONDOKA OLD TRAFFORD.

Uncertainty: Wayne Rooney's future is still up in the air despite his return to training

Uncertainty: Wayne Rooney's future is still up in the air despite his return to training.



Wayne Rooney anatakiwa kuandika na kupeleka barua ya kuomba kuondoka katika klabu yake ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa United yenye maskani yake Old Trafford alirejea jana jumatano mazoezini huku hatma yake ya baadaye bado haifahamiki.
Imefahamika kuwa bado hajakutana na meneja mpya wa klabu hiyo David Moyes kuzungumzia juu ya hali hiyo.
Inadhaniwa kuwa mkutano huo huenda ukafanyika hii leo alahamisi katika kituo cha mazoezi cha cha klabu hiyo Carrington.
Wawili hao wamezungumza lakini si kwa muda mrefu huku ikiarifiwa kuwa msimamo wa United haujabadilika.
Wanasema mshambuliaji huyo wa England hayuko sokoni. Msimamo huo unaonekana kuondoa tetesi za wiki iliyopita kuwa wapinzani wao katika ligi kuu ya England 'Barclays Premier League' Arsenal kuwa walikuwa wakitarajia kupata huduma ya mshambuliaji huyo.
United haikufanya mawasiliano na klabu hata moja ambazo zinadhaniwa kuwa na uwezo wa kumnunua Rooney.
Njia pekee ambayo inaweza kubadilisha hali mambo, ni endapo mchezaji huyo atalazimisha hilo. Wakati wa kuelekea kumalizika kwa msimu uliopita Rooney alipendekeza kwa meneja wa wakati hyuo Sir Alex Ferguson kwamba kuhama kwake kutakuwa ni kuelekea kule anako kupenda.
Maombi ya kimaandishi yatamaianisha kuwa Rooney ataachilia mbali pesa anazodaiwa za kipindi chake cha miaka miwili iliyosalia ya mkataba wake kiasi cha pauni £250,000 kwa wiki.
Frustrated figure: The Manchester United forward has known happier times
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.

All change: David Moyes is shaping his United coaching team
David Moyes

Old Trafford return? Phil Neville could join Moyes at United
Phil Neville huenda akaungana na Moyes United.

Moyes anataka kumchukua mlinzi wa zamani wa United Phil Neville kuungana naye katika timu yake ya ufundi, akiwa na matarajio kuwa Rooney atakubali kusalia huku japo bado kuna mashaka.

Wakati msimu wa usajili wa kiangazi ulipoanza mshambuliaji huyo wa zamani wa Everton alionekana kuanza kujipanga kuanza upya chini meneja aliyemlea wakati alipokuwa Goodison Park.

Wakati Moyes anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza Ijumaa hii huneda ufafanuzi ukatolewa punde.

Rooney anaonekana kutaka kupewa maneno ya kumfariji kutoka ndani ya klabu katika kuondoa hali uhasama kwa lengo la kumlinda na hasira za mashabiki.

No comments:

Post a Comment