MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Senegal, Papiss Cisse anaweza kulazimika kuitema klabu ya Newcastle United
kwasababu ya sakata la mdhamini mpya wa klabu hiyo ambayo ni kampuni ya mikopo
ya Wonga. Nyota huyo ambaye anakadiriwa kulipwa kitita cha paundi 40,000 kwa
wiki, alikuwa akifanya mazoezi mwenyewe baada ya kurejea kutoka katika mapumziko
ya kiangazi wiki iliyopita baada ya kukataa kuvaa fulana yenye nembo ya mdhamini
huyo kwasababu ni kinyume na imani ya dini yake ya Kiislamu.
Chini ya Sharia za Kiislamu,
muumini yoyote wa dini hiyo hatakiwi kunufaika na fedha za mikopo, huku riba
zikiwa hazitolewi katika benki za kiislamu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoolC5k2i6rzZde2tWrK6z6Aa2ELyp161XlVjZJHm_2hEKaYpqM4uYzpmB2qSY4GYzNiqze_-bAlA0v27Ck1YnLhOhjMbPrdXxJScrOsfURDjsKosdOVJaauapwEhbtya0a_XDM9vm4tk/s280/cisse_1494399a.jpg)
Mshambuliaji wa zamani wa West Ham United, Frederic Kanoute ambaye pia ni Muislamu aliruhusiwa na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kufanya fulana isiyokuwa na nembo yoyote wakati klabu hiyo ikidhaminiwa na kampuni ya kamari ya 888.com.
No comments:
Post a Comment