Pages

Tuesday, July 2, 2013

Messi aigwaya Real Madrid, Del Bosque amkingia kifua Casillas na Abramovich atabiriwa kufanya makuu Chelsea




BARCELONA, Hispania

NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi, ameingiwa hofu ya msimu ujao kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa mahasimu wao, timu ya Real Madrid.

Wiki iliyopita Real Madrid ilimtangaza Carlo Ancelotti kuwa kocha wake mpya na nyota huyo anasema kuwa timu hiyo imepata kocha mbadala.

"Tutakabiliwa na upinzani kutoka kwa timu nzuri. Real Madrid ina makocha wazuri na sasa imeongeza mwingine mzuri zaidi," alisema Messi


MADRID, Hispania

KOCHA wa timu ya Taifa ya Hispania, Vincente del Bosque, amesema kuwa hakufurahishwa na jinsi msimu uliopita alivyokuwa akifanyiwa mlinda mlango Iker Casillas, katika timu ya Real Madrid.
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourihno, alikuwa akimsugulisha benchi  Casillas, licha ya nahodha huyo kuonekana kuwa fiti raundi ya pili.

"Nasimama  upande wake," Del Bosque aliliambia gazeti la  Marca. "Watu wanafahamu jinsi nisivyopenda kuingilia masuala ya michezo na sitaweza kufanya hivyo, lakini nasikitika jinsi alivyofanyiwa mambo yasiyo ya kiungwana kijana huyo wa Real Madrid,” aliongeza kocha huyo.



@@@@@@@@@@@@@@@@@

Abramovich atabiriwa kufanya makuu Chelsea
LONDON, England

MWENYEKITI wa Chelsea, Bruce Buck, amesema kuwa mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovich, anafikiria kuipatia mafanikio mengine mengi wakati wakiingia karne ya pili akiwa mmiliki wa timu hiyo.

 Katika kipindi cha miaka 10 tangu aichukue klabu hiyo, Abramovic ameifanya kuwa moja timu tishio katika ukanda wa Ulaya.

Mwaka jana timu hiyo ilionja ladha ya kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na kwa kufanikiwa kumrejesha Jose Mourinho, Buck anasema kuwa raia huyo wa Russia amepanga kufanya makubwa zaidi.


No comments:

Post a Comment