Pages

Sunday, July 7, 2013

IKER CASILLAS NA SARA CARBENERO WATARAJIWA KUPATA MTOTO


 Mlinda mlango wa Hispania na timu ya Real Madrid  Iker Casillas anatarajiwa sasa kuwa baba kwa mara ya kwanza taarifa hizi zikiwa zimethibtishwa na yeye mwenyewe.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32 akiwa na mpenzi wake Sara Carbonero, ambaye ni mwandishi wa habari za michezo kupitia chombo cha habari kinachotambuliak kama Tele 5, wameweka wazi hilo hapo jana wakiwa wamerejea wakitokea katika michuano ya kombe la shirikisho Brazil.

Casillas ambaye hakuwa katika msimu nzuri katika kikosi cha kwanza cha klabu yake ya Madrid chini ya Jose Mourinho alikuwepo langoni katika mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho kule Brazil ambapo walichapwa kwa mabao 3-0. 

Miss Carbonero, naye alikuwepo nchini Brazil kama mwandinshi akifuatialia michezo hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Barajas huko Madrid,  Casillas amesema "nimefurahi sana"

Wawili hao wanasubiri wiki 13 zijazo kuanza kupata mtoto.

No comments:

Post a Comment