Pages

Saturday, June 1, 2013

VITENDO VYA UBAGUZI WA RANGI SASA TIMU KUSHUSHWA DARAJA

Sepp Blatter



Katika hali inayoonekana ni kukomesha kabisa ubaguzi wa rangi Shirikisho la Soka Dunia ni (FIFA) limetangaza adhabu kali ikiwemo ya kushuka daraja timu ambayo itahusika na vitendo vya ubaguzi.

Moja kati ya adhabu itakayotolewa ni faini, kucheza bila mashabiki au kupewa onyo na kama tatizo litaendelea au kujirudia timu itapakonywa alama au kushushwa daraja au kutolewa katika mashindano 
Mkuu wa kuzuia vitendo vya ubaguzi Jeffrey Webb, amesema maamuzi hayo yameafanyika katika wakati muafaka ".
Ameongeza : "Familia yetu ya soka inaelewa kuwa kinachotangazwa sasa katika vyombo vya habari ni asilimia moja tu ya tatizo lenyewe  ambavyo limetokea kwa sasa ulimwenguni.
"Tunatakiwa kuchukua hatua ili katika miaka  20 au  50 ijayo liwe historia kuwa ubaguzi au unyanyasi wa aina hiyo haufai".

FIFA, ambao ndio wanasimamia soka duniani , wamepitisha sheria hii kwa asilimia  99% katika mkutano uliofanyika juzi Mauritius.
.
"Moja kati ya wapinga ubaguzi wa zamani na mfungwa wa maswala ya kibaguzi kutoka Afrika Kusini,  Tokyo Sexwale, ambaye sasa ni mwanachama wa FIFA katika maswala ya ubaguzi amesema kuwa lazima tutazame kwa kutumia kamera nani hakupiga kura kwani kura moja imeharibika katika zile zilizopigwa dhidi ya ubaguzi.

Webb anasema kuwa kupiga kura  kukomesha ubaguzi ni lazima : "Na ningependa kusema hilo ni kosa kwani kura moja haikupigwa ambayo nia aslimia moja tu ya kura zote  1% "
Rais wa FIFA, Sepp Blatter amekubali wazo hilo na kusema tunataka tatizo hili lilikomeshwe kwa kiwango cha sifuri na tunataka kuonyesha kuwa hatutaki jambo hili.
  
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza,  Luther Blissett, ambaye ni balozi wa kupinga ubaguzi wa rangi kwa kutumia kadi nyekundu amekubaliana na hatua hizo.
"kwa maana hii timu yoyote itakayohusika na ubaguzi wa rangi itatolewa katika mashindano Huku Urusi ambayo inaanda Kombe la Dunia inaweza kujikuta ikiaga mashindano itakayoyaanda yenyewe kwani ndio nchini kinara kwa matatizo hayo 














No comments:

Post a Comment