Pages

Monday, June 10, 2013

UJERUMANI YATOLEWA KWENYE MASHINDANO YA VIJANA ULAYA, HISPANIA YASONGA MBELE


Ujerumani imeifuata England kutolewa katika michuano ya Ulaya ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 hatua ya makundi kufuatia goli la dakika za mwisho la Alvaro Morata wa Hispania nchini Israel. 
Mabingwa hao wa mwaka 2009 walikuwa bado na matumaini ya kusonga mbele wakati matokeo yalipokuwa yamesimama sare licha ya kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Uholanzi katika mchezo wa kwanza ambao walifungwa kwa mabao 3-2.
Msimamo wa kundi B wa michuano ya Uefa Under 2013

Played
Won
Drawn
Points





Netherlands
2
2
0
6
Spain
2
2
0
6
Germany
2
0
0
0
Russia
2
0
0
0
Matumaini ya Ujerumani walitoweka kufuatia bao la dakika za lala salama la mshambuliaji wa Real Madrid Morata kunako dakika ya 86.Sasa Hispania  inaungana na Uholanzi ambao wameonyesha dhamira ya kufanya vizuri kufuatia kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Russia iliyokuwa na wachezaji kumi uwanjani katika mchezo mwingine wa kundi B.

No comments:

Post a Comment