Pages

Saturday, June 8, 2013

ROSE PETER AVISHWA TAJI LA RED'S MISS NYAMAGANA BAADA YA DIANA AMIMO KUVULIWA KUTOKANA NA UDANGANYIFU




Hatimaye Rose Peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana baada ya aliyevishwa awali Diana Amimo kuvuliwa kutokana na kudanganya uraia wake.

Shindano la kumsaka mlimbwende wa wilaya ya Nyamagana lililofanyika  Mei 11, mwaka huu katika ukumbi wa JB Belmont Hotel Mwanza na  Diana Amimo kutwaa umalkia na Rose Peter alikuwa mshindi namba 2 na la Miss talent.

Rose amevishwa taji hilo Juni 6, mwaka huu na Mkurugenzi wa Stoppers Entertainment Mukhsin Mambo baada ya Diana kugundulika kuwa alidanyganya uraia wake.

Udanganyifu huo uligundulika na Idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza baada ya maofisa wake kumshikilia na kumhoji wiki moja baada ya shindano hilo kufanyika.

Diana Amimo amevuliwa taji hilo kwa vile vile siyo raia kwani lengo ni kuwashindanisha wazawa wenye umri wa miaka 18 hadi 24.

No comments:

Post a Comment