Pages

Thursday, June 6, 2013

MISS NYAMAGANA 2013 AVULIWA TAJI KISA ...........


Katika hali isiyokuwa ya kawaida lile shindano la kumsaka mlimbwende wa wilaya ya Nyamagana lililofanyika  Mei 11, mwaka huu katika ukumbi wa JB Belmont Hotel Mwanza, limechukua sura mpya baada ya aliyeshinda taji hilo Diana Amimo kuvuliwa umalkia na kumvisha  Rose Peter ambaye alikuwa mshindi namba 2 na la Miss talent.

Kulingana na chanzo chetu cha habari ambae alikuwa ni mmoja wa warembo hao amesema kuwa Diana Amimo amevuliwa taji hilo kwa vile hakuwa  mtanzania hivyo hakusitahili taji hilo kwani lengo ni kuwashindanisha wazawa na si wageni kutoka nje ya nchi

Kiukweli kaka hata sisi ilitushangaza sana mimi Diana namjua kwao si Tanzania bali anatoka( ) na alikuja mwanza kwa dada yake ambaye naye si mtanzania, lengo lake kubwa ilikua aje atafutiwe kazi na huyo dada yake lakini kwa kuwa Diana ni mrembo alijipenyeza na kuingia Miss Nyamagana hata waandaaji walilijua hilo kabla, sisi tukajua lazima watamchuja ila tukashangaa kapeta hadi kabeba taji kiukweli ilituuma sana nashukuru ukweli umejulikana now I’m happy…..kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo watu waliohudhuria shindano hilo walihoji kwanini Rose aliekua na sifa zote hakuchukua na wamemvisha Diana ambae hata kimuonekano hakusitahili kunyakua taji hilo.

No comments:

Post a Comment