Pages

Tuesday, June 4, 2013

JOSE MOURINHO ASAINI MIAKA MINNE(4) NA KLABU YAKE YA ZAMANI CHELSEA

karibu mjini tena "The Special One" karibu nyumbani

Mourinho sasa yu wa Chelsea kwa mara nyingine tena, Rasmi kuanza Ziara ya kabla Msimu mpya kuanza Mwezi Julai huko Barani Asia Nchini Thailand, Malaysia na Singapore na kisha kusafiri kwenda Marekani kushiriki Mashindano ya International Champions Cup yatakayoshirikisha pia Klabu mbili ambazo Mouronho aliwahi kuwa Bosi, Real Madrid na Inter Milan, pamoja na Everton, Juventus, AC Milan, Valencia na LA Galaxy.

Ujio huu wa Jose Mourinho Stamford Bridge kwa mara ya pili, baada ya kuwa hapo kati ya Miaka 2004-2007 na kutwaa Makombe 6, unaleta mategemeo makubwa kwa Wadau wa Klabu hiyo.

Jose Mourinho akiwa amanyanyua jezi ya Chelsea juu ambapo amerudi kwa mara nyingine kama meneja wa klabu hiyo ya Chelsea
Kwa mara nyingine tena..

Karibu .... karibu... Mourinho nyumbani jisikie kwa mara nyingine tena.
Jose Mourinho amesaini miaka minne na klabu ya Chelsea leo hii.

Mara ya mwisho Jose Mourinho akiwaaga mashabiki kwenye mechi ya mwisho kabla ya kutua Darajani

Enzi hizo: Mourinho aliposhinda kombe la ligi kuu akiwa bosi wa Chelsea kipindi hicho..

Demba Ba ataungana na Mourinho kwa staili ya aina yake

Mimi na wewe tena!!! Mourinho ataungana tena na Roman Abramovich ambapo pia walikuwa pamoja hapa kama unavyowaona kwenye picha ya 2004 kabla hajaondoka mtu mzima na wa kipekee.

Sauti za mashabiki darajani zilikuwa zikimlialia Mourinho kuja ili Rafa Benitez aondoke Stamford Bridge na sasa imetimia...karibu sana "The Special One"Mtanikoma sasa narudi Stanford Bridge, tutachinjana live...!!

Sisi tunamtaka Jose hakuna jingine!!!!

MOURINHO'S CHELSEA ROLL OF HONOUR 2004-2007
Premier League (2): 2004-05, 2005-06
FA Cup (1): 2006-07
Football League Cup (2): 2004-05, 2006-07
FA Community Shield (1): 2005

No comments:

Post a Comment