Pages

Wednesday, June 5, 2013

CHEKI BAADHI YA PICHA ZA MAPOKEZI YA MWILI WA NGWEA MOROGORO

Hapa ni Miembe 7 karibu na Mlandizi Pwani, hawa ni baadhi ya mashabiki wa marehemu Ngwea waliojitokeza barabarani kuuaga mwili wa marehemu. Wakati huo huo wananchi wa maeneo ya Mikese, wamekusanyika na kuusimamisha msafara uliobeba mwili wa marehemu Ngwea kwa kutaka na wao wamuage, akizungumza na Cloud Fm "Moe Fire" amesema walikutana na kundi la watu nakudhani labda kuna tatizo. Baada ya kusimamishwa na trafic na kuuliza tatizo ni nini, Trafic alisema kuwa wananchi hao wamekusanyika ili kuuaga mwili wa marehemu Ngwea na kudai kitendo hicho kikifanyika ndio amani itapatikana.

Kilichofanyika ni kuruhusu watu wale walishike gari lililokuwa na mwili wa Ngwea na kuondoka, lakini baada ya kuondoka, zaidi ya pikipiki 50 walizozikuta pale ziliongoza msafara huku magari mengine pia yakiunga msafara huo.
Mama mzazi wa marehemu Albert Mangwea akiwa hoi kitandani kwa mshtuko alioupata kutokana na kifo cha mwanae
Sehemu ya umati mkubwa wa watu wajitokeza kupokea mwili wa Albert Mangwea Morogoro

Masanja mkandamizaji akiwa na Zola D nyumbani kwa Mama Albert Mangwea Morogoro

No comments:

Post a Comment