Pages

Tuesday, May 14, 2013

ZAMALEK NA AL AHALY WAPANGWA KUNDI MOJA KLABU BINGWA AFRIKA


Cairo rivals to clash again in 2013 Orange CAF Champions League group stage

 
Kwa mara ya pili na kwa mwaka wa pili mahasimu wa soka la Misri  Zamalek na Mabingwa watetezi  Al Ahly wamewekwa tena katika kundi moja katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani afrika maarufu kama Orange CAF Champions League katika ratiba iliyopangwa leo katika makao makuu yaCAF huko Cairo. Mafahali hao wawili wa Misri wapo kundi A na watakutana  katika mechi ya ufunguzi wa makundi hayo ambayo ndiyo itakayo kuwa mechi ya kwanza 19-21st Julai huku  Zamalek wakiwa wenyeji wa mchezo huo. 
Mabingwa wa mwaka 1995 Orlando Pirates wataialika  AC Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo katika mchezo wa kundi A .
 
 
Kocha msaidizi wa  Zamalek, Ossama Nabuih amesema kuwa  sio jambo la kushangaza kuwa kundi moja na mahasimu wao wakubwa  Al Ahly kwa mara ya pili . “ tuliitarajia ratiba hii . hakuna kusema kuwa kundi hili ni rahisi au ngumu . Kwa hatua hii kila kundi ni gumu tuna kwenda kucheza kwa kujiamini na tutafuzu katika kundi hili ” . kundi letu ni gumu kuliko jingine  . Tutakutana na timu ngumu kutoka katika mataifa tofauti .anamaliza  Nabuih          



Group A
Al Ahly  (Egypt)
AC Leopards (Congo)
Orlando Pirates (South Africa)
Zamalek (Egypt)
 
 
Group B
Esperance (Tunisia)
Coton Sport (Cameroon)
Recreativo de Libolo (Angola)
Sewe Sport (Ivory Coast)

No comments:

Post a Comment