KARIBIA kila msimu wa usajili, imekuwa ikishuhudiwa
wachezaji aidha wawe na umri mkubwa ama mdogo, wakisajiliwa kwa gharama kubwa.
Gharama hiyo imekuwa ikitokana na uwezo wa kila
mchezaji ama kadiri jinsi anavyoivutia timu inayomuhitaji.
Katika makala haya, tunaangalia wachezaji waliowahi kusajiliwa
kwa bei kubwa wakiwa na umri zaidi ya miaka 30, walipokwenda kujiunga na klabu mpya.
5. Angelo Peruzzi - Inter Milan kwenda Lazio -pauni mil. 10.5.
Akiwa ameitumikia msimu mmoja Inter Milan, mlinda mlango
huyo raia wa Italia, alijiunga na timu ya Lazio ambako alimalizia muda wake wa
soka ikiwa ni baada ya kuonekana uwanjani mara 200.
Mbali na timu hizo mlinda mlango huyo mzoefu, pia aliwahi
kuzichezea timu za AS Roma na Juventus kabla ya majeraha kumfanya atundike
daluga mwaka 2007.
4. Zlatan Ibrahimovic
- AC Milan kwenda Paris Saint Germain -pauni mil. 15.7
Akiwa ameshatwaa ubingwa na klabu mbalimbali akiwa
na timu za Ajax, Juventus, Inter, Barcelona na AC Milan, hatimaye mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Sweden,
aliamua kujiunga na timu ya PSG.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa aking’ara
akiwa na klabu hiyo ya Rossoneri kabla
ya kwenda kwenye klabu hiyo matajiri wa jijini Paris.
Licha ya kujiunga na
klabu mbalimbali, mshambuliaji huyo mzaliwa wa Jiji la Malmo anaonekana kuwa
mwenye mafanikio na msimu huu ameshafunga mabao 32 katika ligi hiyo ya Ligue 1.
3. Claude Makelele - Real Madrid kwenda Chelsea -pauni mil. 16.8.
Katika msimu huo ambao Blues ilitumia zaidi ya pauni milioni
zaidi ya 100, Mfaransa huyo alijikuta akitua Stamford Bridge akiwa na wachezaji
wengine wa kimataifa kama vile, Juan Sebastian Veron, Adrian Mutu na Hernan
Crespo.
Akiwa katika msimu wake wa kwanza na Klabu hiyo ya jijini
London, ambayo kwa bahati mbaya ilimaliza msimu huo ikiwa nafasi ya pili lakini
baadaye, Makelele alinoga mikononi mwa
Jose Mourinho, ambaye aliiongoza Chelsea
kutwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu na kisha mchezaji huyo akaonekana
kuwa shujaa kwenye michuano hiyo.
2. Samuel Eto'o - Inter Milan kwenda Anzhi
Makhachkala -Pauni mil.18.4
Hiyo ndiyo siku ambayo nyota huyo wa zamani wa Barcelona,
alipofahamika kuwa ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi duniani baada ya
kusaini mkataba unaomruhusu kuingiza pauni milioni 15.3 kwa mwaka
.
.
1. Diego Milito - Geno kwenda Inter Milan - euro mil.30
Akiwa na klabu hiyo ya Nerazzurri, raia huyo wa Argentina
aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia msimu wa 2009-10
akiwa chini ya Jose Mourinho.
Katika msimu huo, aliweza kufunga mabao 30 mawili akiwa
ameyafunga kwenye mechi ya fainali ya michuano ya Klabu Bingwa.
Kutokana na kiwango hicho, mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 33, alipongezwa ingawa hajarudia tena kuonesha kiwango hicho na msimu huu
anakabiliwa na majeraha ya goti.
No comments:
Post a Comment