SIR ALEX FERGUSON ALAMBA TUZO YA MENEJA BORA WA MWAKA. NI TUZO YA 11 YA NAMNA HIYO!
CHAMA cha Makocha wa Ligi
Kuu nchini Uingereza kimemteua Aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester United,
Sir Alex Ferguson kuwa meneja bora wa mwaka wa ligi hiyo. Ferguson ambaye
amestaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha United kwa kipindi
chamiaka 26 anakuwa kocha wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara nyingi zaidi ambayo
hupigiwa kura na makocha wenzake. Akipokea tuzo yake kutoka kwa meneja wa West
Ham United Sam Allardyce katika sherehe hizo jana usiku, Ferguson alitania kuwa
mmiliki wa West Ham Steve Clarke anatakiwa naye apewe tuzo kwa timu yake
kuifunga United mabao matano katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa
Jumapili. Ferguson amesema sare ya mabao 5-5 waliyopata dhidi ya West ham kila
atakuwa akiikumbuka kwa kipindi kirefu kijacho na kwa upande mwingine anashukuru
amemaliza kazi hiyo ya ukocha kwasababu ni moja ya shughuli ngumu kabisa
duniani.
No comments:
Post a Comment