Pages
▼
Sunday, May 19, 2013
SIR ALEX: BISKUTI NDIO UGONJWA WANGU
MANCHESTER, England
KOCHA mstaafu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amebainisha kwamba yeye ni dhaifu mkubwa wa biskuti za chocolate.
Mskochi huyo, ambaye amekuwa maarufu zaidi kutokana na kutafuna bazoka anapokuwa kwenye benchi lake wakati wa mechi za timu zake, alisema amekuwa akitumia muda mwingi wa kujifunza masuala ya jikoni na kuwa mtaalamu wa jambo hilo.
Ferguson alitangaza kustaafu ukocha baada ya kudumu kwa miaka 26 katika kibarua cha kuinoa Man United, yenye maskani yake Old Trafford.
"Biskuti ndio udhaifu wangu," Daily Mail lilimnukuu Ferguson akisema. "Caramel wafers, Kit Kats na Jaffa Cakes. Najaribu kuvuta hisia ya ladha yake.
"Nilikuwa mpishi kwa mwaka mmoja na nusu. Nilipata eneo Paisley kujenga mgahawa, nilikuwa meneja wa St Mirren kwa kipindi hicho.
"Nilisema kama nitakuwa na mgahawa, nitahitaji kufahamu jiko linavyofanya kazi. Nilikuwa nikiitwa Beechwood. Nilikuwa mahiri kwenye hilo na pia ni mpishi mzuri wa vyakula vya Kichina."
Ferguson amestaafu kuinoa Man United, nafasi ambayo kwa sasa amechukua David Moyes, ambaye ataanza rasmi kibarua chake Old Trafford kuanzia Julai Mosi.
No comments:
Post a Comment