Pages

Friday, May 31, 2013

SIMBA YAKAMILISHA MAZUNGUMZO NA MUSA OLOYA, SASA KUTUA MSIMBAZI NA KUFANYA SIMBA KUWA NA WAGANDA WANNE

MCHEZAJI wa kimataifa wa Uganda Cranes, Musa Oloya huenda akatua Simba Sports Club kwa msimu ujao kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba ambayo ilivuliwa ubingwa msimu wa  2012/13 sasa inajiandaa kwa mashindano ya Kombe la Kagame (CECAFA)  iliyopangwa kufanyika Sudan mwezi ujao.
Timu hii pia  inajengwa upya kwa ajili ya msimu ujao na kuzipa pengo la  wachezaji waliondoka kama winga Mrisho Ngassa ambaye amejiunga mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania , Yanga.

mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe alithibitisha majadiliano yapo hatua ya juu na nyota wa Uganda ambaye yupo katika kikosi cha Uganda Cranes.
Oloya, ambaye zamani alikuwahi kuchezea Saigon Thanh Xuan wa Vietnam, anatarajiwa kujiunga na Simba ya Tanzania baada ya Cranes kucheza mchezo wa  kirafiki na Libya na wa kufuzu Kombe la Dunia 2014  mwezi ujao.

Oloya atajiunga  na mwenzake toka Uganda Samweli Ssekoom ambaye alikuwa mchezaji wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) ambaye amesaini Simba maarufu kama Msimbazi Street.
Simba hadi sasa ina wachezaji wa tano kigeni, ambao ni pamoja na Kipa Abel Dhaira na  Mude Mussa  (Uganda), Felix Sunzu (Zambia)

Simba pia imewasajili beki Issa Rashid,(baba Ubaya)  mlinzi Andrew Ntalla, mshambuliaji Zahor Pazi na kiungo Twaha Shekuwe.

Simba ilishika nafasi ya tatu katika msimu uliomalizika 2012/13 nyuma ya Yanga FC washindi na nafasi ya  pili ilichukuliwa na  Azam. 

No comments:

Post a Comment